Amos 4:1-6

Israeli Hajarudi Kwa Mungu


1 aSikilizeni neno hili, ninyi ng’ombe wa Bashani
mlioko juu ya Mlima Samaria,
ninyi wanawake mnaowaonea maskini,
na kuwagandamiza wahitaji,
na kuwaambia wanaume wenu,
“Tuleteeni vinywaji!”

2 b Bwana Mwenyezi ameapa kwa utakatifu wake:
“Hakika wakati utakuja
mtakapochukuliwa na kulabu,
na wanaosalia kwa ndoana za samaki.

3 cNanyi mtakwenda moja kwa moja
kupitia mahali palipobomolewa kwenye ukuta,
nanyi mtatupwa nje kuelekea Harmoni,”
asema Bwana.


4 d“Nendeni Betheli mkatende dhambi;
nendeni Gilgali mkazidi kutenda dhambi.
Leteni dhabihu zenu kila asubuhi,
zaka zenu kila mwaka wa tatu.

5 Mchome mkate uliotiwa chachu kama sadaka ya shukrani,
jisifuni kuhusu sadaka zenu za hiari:
jigambeni kwa ajili ya sadaka hizo, enyi Waisraeli,
kwa kuwa hili ndilo mnalopenda kulitenda,”
asema Bwana Mwenyezi.


6 e“Niliwapa njaa kwenye kila mji,
na ukosefu wa chakula katika kila mji,
hata hivyo bado hamjanirudia mimi,”
asema Bwana.

Copyright information for SwhKC